Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 3:58:25
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
Episódios
-
-
Wanaharakati wataka uhifadhi wa msitu wa mvua wa Kongo kupewa kipaumbele
26/12/2025 Duração: 09minMisitu ya mvua barani Afrika kimsingi imejikita katika Bonde kubwa la Kongo, msitu wa pili kwa ukubwa duniani wa kitropiki, unaohifadhi wanyamapori wa kipekee kama sokwe, na tembo wa msituni, pamoja na maeneo mengine muhimu kama vile Misitu ya Guinea ya Afrika Magharibi, misitu ya Afromontane Mashariki, na misitu ya pwani kutoka Kenya hadi Msumbiji yenye misitu ya kipekee ya kisiwa cha Madagaska. Mifumo hii muhimu ya ikolojia inakabiliwa na vitisho kutoka kwa ukataji miti, kilimo, na kuathiri bioanuwai yao tajiri. Kutokana na vitisho hivi wanaharakati wamepaza sauti za kulindwa kwa misitu ya mvua.
-
Lugha ya kiswahili katika kuimarisha uelewa, uhamasishaji na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi
19/12/2025 Duração: 10minWakati viongozi wa dunia, wanasayansi na watunga sera wanapokutana katika miji mikuu ya Dunia kujenga hoja kuhusu hatima ya sayari kupitia mikutano ya tabianchi ya Umoja wa Mataifa, Wataalamu wa lugha,, walimu pamoja na wanafunzi waaendeleza mijadala. Kaulimbiu ukiwa ni namna lugha adimu ya kiswahili inavyotumika katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
-
Kituo cha jambo Redio nchini DRC chapokea tuzo kwenye COP30
15/12/2025 Duração: 10minNchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kituo cha Jambo redio, kimejitwika jukumu la kuelimisha jamii kuhusu masuala ya mazingira na tabianchi, lakini muhimu sana ni haki zao. Katika mkutano wa tabianchi uliotamatika jijini Belem nchini Brazil, kituo cha Jambo Redio kilipokea tuzo kutoka kwa shirikika linalotetea haki za wanawake Women Engage for a Common Future, WECF. Kituo hiki, kimekuwa kikitoa habari kwa jamii ambazo wakati mwingine hazina uwezo wa kupata habari.
-
COP30 uliotamatika jijini Belem, Brazil,, suala la ufadhili wa tabianchi, nishati safi ni miongoni mwa ajenda
05/12/2025 Duração: 09minMiongoni mwa mambo yalioamuliwa ni kuhamasisha kiasi cha fedha trilioni 1.3 kila mwaka kufikia 2035 wa ajili ya hatua za tabianchi, kuimarisha fedha uhimilivu mara tatu kufikia 2035. Msikilizaji, suala la kuharakisha ufadhili wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inasalia kuwa kipaumbele cha dharura hasa kwa nchi zinazoendelea ambazo zina athirika pakubwa na janga hilo.
-
Shirika la Weather Mtaani labuni teknolojia ya kuepuka majanga ya hali ya hewa Kibera
18/11/2025 Duração: 09minMvua huja kwa sauti ya baraka lakini katika kitongoji, sauti hiyo hubeba hofu. Maji yanapoteremka kutoka angani, katika sekunde chache, barabara hugeuka mito. Vyumba vya kulala vinageuka mabwawa. Katika kitongoji cha Kibera jijini Nairobi nchini Kenya, hali hiyo ya hofu imebadilishwa kupitia kundi la vijana linalojiita Weather Mtaani. Shirika la Weather Mtaani linatumia teknolojia ya simu kutafsiri jumbe za utabiri wa hali ya hewa kutoka kwa mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa ya Kenya, kwa lugha inayoeleweka.
-
Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi COP30 jijini Belem, Brazil
12/11/2025 Duração: 09minMkutano huu unakwenda kufanyika wakati ripoti mpya ya shirika la mazingira la umoja wa mataifa UNEP, ikionesha kuwa bado dunia iko nyuma katika kuafikia malengo ya mkataba wa Paris wa kudhibiti wastani wa jotoridi duniani kufikia nyuzijoto 1.5.
-
Ripoti: Matajiri wachache wanateka nyara dunia kwa kuchangia pakubwa utoaji wa hewa ukaa
06/11/2025 Duração: 09minDunia inapojiandaa kwa mkutano wa kimataifa wa Mazingira COP30 utakaofanyika Belém, Brazil, ripoti mpya imeibua mjadala mkali—si tu kuhusu uzalishaji wa hewa ukaa, bali pia kuhusu ukosefu wa usawa. Utafiti mpya wa shirika la Oxfam, unaonesha kuwa mataifa tajiri na watu wachache wenye utajiri mkubwa wanachangia kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabianchi. Inaitwa “ukosefu wa haki wa hali ya hewa.” Mtaalam wetu leo kulichambua hili ni David Abudho, anayeshughulika na mabadiliko ya tabia nchi barani Afrika kutoka shirika la Oxfam.
-
Siku ya Chakula duniani: Mapendo Banque Alimentaire yapambana na ukosefu wa usalama wa chakula
24/10/2025 Duração: 10min -
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga
18/10/2025 Duração: 09minRipoti ya 2025 ya tathmini ya kidunia juu ya kupunguza hatari za majanga inakadiria kuwa gharama kamili ya kukabili majanga ni karibu dola trilioni2.3, na licha ya uwekezaji huu, bajeti za kitaifa bado ni za kiwango cha chini mno.
-
Vijana walioasi uhalifu na kujitosa katika kutunza mazingira ya kijiji chao
07/10/2025 Duração: 10minFahamu kundi la vijana kutoka mtaa wa korogocho jijini Nairobi, walioasi uhalifu na kuamua kutunza mazingira ya jamii yao. Vijana hawa wananuia kuwa mfano kwa kizazi kijacho kufahamu kuwa hata juhudi ndogo zinaweza kuleta mabadiliko katika jamii inayowazunguka.
-
Siku ya kimataifa ya hamasisho kuhusu upotevu na uharibifu wa chakula
29/09/2025 Duração: 09minWakati mamilioni ya watu wanalala njaa kila siku, chakula kizuri hutupwa mashambani, katika maduka makubwa, mikahawa - na ndiyo, hata katika nyumba zetu wenyewe. Uharibifu wa chakula sio tu kuhusu kile kilicho kwenye sahani zetu. Pia inahusu rasilimali zinazotumiwa kuzalisha chakula hicho: maji, ardhi, nishati, na raslimali watu, zote hupotea wakati chakula kinaharibika.
-
ACS2: Addis Ababa: Vijana wasisitiza uwekezaji kwenye ajira za kijani
29/09/2025 Duração: 10minUchumi wa kijani ni miongoni mwa mada kuu zilizojadiliwa kwenye mkutano wa pili wa mazingira wa bara la Afrika uliofanyika hivi majuzi jijini Addis ababa, ambapo wajumbe walijadili mikakati ya kufadhili maendeleo ya kijani barani Afrika kupitia masuluhisho yanayotegemea asili, teknolojia safi. Mjadala umeibuka kuhusu nafasi ya vijana katika mipango ya serikali za Afrika kuelekea uchumi wa kijani, kupitia ajira za kijani.
-
Oxfam: Nchi tajiri zimevunja ahadi zao za ufadhili wa hali ya hewa kwa Afrika
10/09/2025 Duração: 09minRipoti mpya ya shirika la kimataifa ya Oxfam inasema kuwa nchi tajiri zimetoa tu asilimia 4 pekee ya fedha zinazohitajika Afrika Mashariki kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa. Nchi za Afrika Mashariki ni miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi na mzozo wa hali ya hewa, licha ya kuchangia asilimia 0.09 ya uzalishaji wa hewa ukaa duniani.
-
Wiki ya maji duniani na mabadiliko ya tabianchi: Changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo kame
01/09/2025 Duração: 09min -
Vijana Dar es Salaam watumia teknolojia kukabili mafuriko na mabadiliko ya tabianchi
26/08/2025 Duração: 09min -
Mtokeo ya majadiliano ya kimataifa kuhusu mkataba wa kisheria wa kukabili taka za plastiki
20/08/2025 Duração: 09minKwa mara nyingine tena, dunia ilipoteza fursa muhimu ya kuwa na mkataba huo, majadilianao yakigonga mwamba kutokana na nchi kutofautiana kwenye baadhi ya maandishi.
-
UN: Ni asilimia 35 pekee ya malengo ya maendeleo endelevu ndio yako katika njia sahihi kufikiwa
11/08/2025 Duração: 09minRipoti ya malengo ya maendeleo endelevu mwaka 2025, ikiwa ni miaka kumi tangu mataifa kuanza kufanyia kazi malengo hayo. Katika ripoti hiyo, UN inasema dunia bado iko nyuma katika kuhakikisha malengo hayo 17 yanaafikiwa kikamilifu kufikia mwaka wa 2030.
-
Mkataba wa plastiki: Mgawanyiko kuhusu jinsi ya kukabiliana na hatari ya kiafya na kiikolojia.
05/08/2025 Duração: 09minMataifa mbalimbali ulimwenguni yameombwa kuchukua hatua na kutatua mzozo wa kimataifa wa plastiki, mwenyekiti wa kamati ya majadiliano ya kiserikali, mwanadiplomasia wa Ecuador, Luis Vayas Valdivieso akiwaomba wadau waliokusanyika Geneva, Uswizi kwa siku 10 kuunda mkataba wa kihistoria wa kuzuia uchafuzi wa plastiki. "Uchafuzi wa plastiki unaharibu mazingira, unachafua bahari na mito yetu, unatishia viumbe hai, na unadhuru afya ya binadamu," alisema Valdivieso. Wataalam pia katika ripoti iliyochapishwa kwenye Jarida la matibabu la Lancet, wameonya kuwa uchafuzi wa plastiki ni "hatari kubwa, inayokua na isiyotambulika" kwa afya ambayo inagharimu dunia angalau dola trilioni 1.5 kwa mwaka. Bonyeza hapo juu kusikiliza wito wa watetezi wa mazingira kuhusu umuhimu wa kupatikana kwa mkataba wa plastiki.
-
Matokeo ya mkutano wa AMCEN katika jitihada za bara la Afrika kukabili mabadiliko ya tabinanchi
28/07/2025 Duração: 09minKenya ilikuwa mweneyeji wa mkutano wa 20 wa mawaziri wa mazingira kutoka mataifa ya Afrika, AMCEN, mkutano muhimu kuelekea mikutano ya kimataifa kuhusu mazingira kama vile COP30, INC5.2 na UNEA-7.