Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Hatau ya Marekani kujiondo kwenye mikataba ya mazingir na tabianchi na athari zake

Informações:

Sinopse

Aliporejea madarakani Januari 20 2025, kwa mara ya pili Trump aliiondoa Marekani katika mkataba wa tabianchi wa Paris wa 2015. Mwaka wa 2025, Washington haikuwatuma maafisa wake wa juu katika mkutano wa tabianchi wa COP30, uliofanyika Belem, Brazil. Na sasa wiki chache zilizopita, utawala wa Trump ulitangaza kuiondoa Marekani katika mashirika 66 ya kimataifa, ikiwemo ile ya UNFCCC.