Afrika Ya Mashariki

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editora: Podcast
  • Duração: 3:57:31
  • Mais informações

Informações:

Sinopse

Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.

Episódios

  • Hofu kwa wavuvi wa biashara ya samaki Ziwa Victoria nchini Tanzania

    28/08/2024 Duração: 09min

    Serikali ya Tanzania imekuwa ikiteleza kanuni za mwaka 2009 juu ya kulifunga ziwa hilo kwa muda wa siku 10 utaratibu huu umekuwa endelevu hadi sasa ambapo kila mwezi wavuvi hawaruhusiwi kujishughulisha na shughuli za uvuvi kwa siku 10, ikiwa na maana kwamba katika kipindi cha mwaka mzima, Ziwa hilo linafungwa kwa siku 120, sawa na Robo mwaka yaani miezi minne

  • Shughuli za uvuvi zarejelewa katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma

    23/08/2024 Duração: 09min

    Shughuli za Uvuvi katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma zilifungwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Mei 15 hadi Agosti 15, mwaka huu lengo likiwa ni kupumzisha ziwa hilo, ili kuchagiza ongezeko la SamakiKufungwa kwa ziwa hilo ni makubaliano yaliyoazimiwa katika kikao kilichofanyika mwaka 2022 kikihusisha nchi zinazozunguka ziwa hilo ambazo ni Zambia, Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)

  • Namna siku ya vijana ilivyoadhimishwa katika nchi za Afrika Mashariki

    14/08/2024 Duração: 09min

    Siku ya Vijana Ulimwenguni, ambayo huadhimishwa tarehe 12 Agosti kila mwaka, ilianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka wa 1999 kupitia maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Lengo kuu la siku hii ni kutambua mchango wa vijana katika jamii, kuhamasisha ushirikiano na kuunga mkono haki za vijana, na kuonyesha jinsi vijana wanavyoweza kuchangia maendeleo endelevu na amani duniani

  • Uchaguzi wa urais uliofanyika nchini Rwanda ambapo rais Kagame alitangazwa mshindi

    20/07/2024 Duração: 09min

    Karibu katika Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwama nchini Rwanda tukianga zoezi la kupiga kura lilifanyika Julai 14 na 15, 2024.

página 2 de 2