Jukwaa La Michezo

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editora: Podcast
  • Duração: 9:28:53
  • Mais informações

Informações:

Sinopse

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali. 

Episódios

  • Yanga yashinda ubingwa wa 26 huku CAF ikitoa ratiba rasmi ya michuano ya Chan

    28/06/2025 Duração: 23min

    Tuliyokuandalia leo ni pamoja na Yanga kushinda ubingwa wao wa 26, klabu ya Les Aigle du Congo yashinda ubingwa wa ligi ya DRC, historia zilizowekwa na Faith Kipyegon na Khaman Maluach wiki hii, Aish Manula arejea kikosini Taifa Stars kuelekea Chan, nini sababu ya vilabu vyote vya Afrika kubanduliwa kwenye kombe la dunia la vilabu? Ligi kuu ya Uingereza kuleta mabadiliko mapya mapumzikoni msimu ujao, Pogba,Giroud warejea katika ligi ya Ufaransa huku Lyon ikishushwa kutokana na matatizo ya fedha

  • Fainali ya CHAN 2024 kuchezwa Kenya, mechi ya ufunguzi kupigwa Tanzania

    21/06/2025 Duração: 24min

    Tuliyokuandalia leo ni pamoja na CAF kutangaza viwanja vitakavyoandaa michuano ya CHAN, kombe la CECAFA kwa kina dada, DRC yakuwa mshiriki rasmi wa AC Milan, matokeo ya Paris Diamond League na Mauritius 7s. Matokeo ya vilabu vya Afrika kwenye raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia la Vilabu huku mshindi wa French Open Carlos Alcaraz akifuzu nusu fainali yake ya saba mwaka huu kwenye tenisi.

  • Kipkeino Classic: Lachlan Kennedy aibuka mshindi wa mbio za mita 100

    31/05/2025 Duração: 23min

    Tuliyokuangalia leo ni pamoja na matokeo ya riadha za Kipkeino Classic, mkutano mkuu wa FKF, tuzo za soka Rwanda, APR yasajili mchezaji Omot kuelekea fainali za BAL, DRC yajiandaa mechi za kirafiki kuelekea WAFCON, uchambuzi wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

  • CAF: Simba kuchuana na RS Berkane leo kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho

    17/05/2025 Duração: 23min

    Leo tumekuandalia mengi ikiwemo fainali ya kombe la shirikisho la CAF kati ya Simba na RS Berkane, fainali za Afcon U20, Congo Brazaville yarejeshwa katika soka ya kimataifa, droo kamili ya michuano ya Chan 2024, mkondo wa Nile katika ligi ya basketboli ya Afrika, tuzo za wanasoka bora ligi kuu ya Uingereza.

página 2 de 2